Sunday, September 14, 2014

Picha na Habari Kamili:ZAIDI ya waathirika 1000 wa milipuko ya mabomu ya Mbagala Kuu iliyotokea jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wanatarajia kuitisha mkutano wa hadhara wa kuwaondoa madarakani viongozi wao wa serikali ya mtaa kwa madai ya kushindwa kusimamia madai ya kupunjwa fidia ya majengo.


Picha na Habari Kamili:ZAIDI ya waathirika 1000 wa milipuko ya mabomu ya Mbagala Kuu iliyotokea jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wanatarajia kuitisha mkutano wa hadhara wa kuwaondoa madarakani viongozi wao wa serikali ya mtaa kwa madai ya kushindwa kusimamia madai ya kupunjwa fidia ya majengo.

 Hundi ambazo siyo sahihi kwa malipo ya waliopoteza nyumba wa watu na mali huu siyo Ubinadamu madaraka yana mwisho.

 Wanasikitika kwa kutotendewa haki ya kibinaadamu.

 Wananchi wa Mbagala Kuu Waathilika na Mabomu wanaamini wametolewa Kafara kwa viongozi waliosimamia malipo kwa kunufaika kupitia matatizo yao.

 Mh. Rais wananchi wanasema toka ulipokwenda mbagala Kuu februari 2010 hakuna kilichofanyika zaidi kulipwa kiasi cha Tsh 1,400 na 1950 fidia ya nyumba je hii ndiyo HAKI? Rais.

 Wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kulalamikia malipo ya dhuluma.

Wananchi wa Mbagala Kuu ambao waliathilika na mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ),  Aprili 2009 wakiwa na mabango yenye ujumbe wa kumtaka Rais Jakaya Kikwete asikilize kilio chao baada ya kufanyiwa unyama na viongozi waliosimamia zoezi la malipo yao.
---

Na Asha Mwakyonde


ZAIDI ya waathirika 1000 wa milipuko ya mabomu ya Mbagala Kuu iliyotokea jijini Dar es Salaam mwaka 2009, wanatarajia kuitisha mkutano wa hadhara wa kuwaondoa madarakani viongozi wao wa serikali ya mtaa kwa madai ya kushindwa kusimamia madai ya kupunjwa fidia ya majengo.



Wamesema licha ya miongoni mwao kulipwa fidia ya shilingi 1,400 kwa  nyumba bado viongozi wao wa mtaa wameendelea kuwa kimya katika kufuatilia fidia halisi tangu janga hilo la mabomu liwakute miaka minne iliyopita.



Wakazi hao wa Mbagala Kuu, walitoa kauli hiyo jana walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari na kusema wamefikia uamuzi huo baada ya kukosa imani na viongozi wao.

Akizungumza kwa niaba ya waathirika wa mabomu hayo katibu wa Kamati ya Waathirika, Thomas Mbasha, alisema madai yao ni pamoja na kulipwa fidia ndogo na kwamba hata baada ya kuandika barua ya malalamiko  kwa serikali wakitaka kuongezwa fidia lakini hawajapata majibu yenje tija. 



"Tumeandika barua kadhaa kwa serikali ikiwa ni pamoja na Rais tukiomba fidia zetu lakini hakuna kilichofanyika,tunahitaji Rais aingilie kati suala hili na kutusaidia ili tulipwe stahili zetu kabla hajaondoka madarakani," alisema Mbasha. 



Alisema fidia walizolipwa awali hazilingani na thamani ya mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo huku akiainisha fidia ya kiwango cha juu walicholipwa ni shilingi 4900 . 



Awali  Mwenyekiti wa Kamati ya waathirika wa mabomu ya Mbagala kuu, Stephen Gimonge, alisema Rais Jakaya Kikwete, alitembelea eneo hilo na kuahidi kuwa serikali itawalipa fidia inayostahili lakini ahadi hiyo haijazaa matunda. 



Alisema wakati wa ziara yake kwa waathirika wa milipuko ya Mbagala Rais Kiwete alimuelekeza Waziri Mkuu kuhakikisha fidia inatolewa  kulingana na mali  zilizopotea.



 Hata hivyo waathirika hao walimuomba Kikwete kuingilia kati ili awasaidie waweze kupata fidia inayostahili kutokana na mali na vitu vyao vilivyoharibiwa wakati wa tukio hilo lililotokea Aprili 2009.