Sunday, September 14, 2014

Hebu Jionee Picha Mbalimbali Jinsi Mbunge wa Kawe - Chadema Halima Mdee Alivyoshinda Kwa Kishindo Uchaguzi Kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema na Kuwa Mwenyekiti Rasmi wa Bawacha



Hebu Jionee Picha Mbalimbali Jinsi Mbunge wa Kawe - Chadema Halima Mdee Alivyoshinda Kwa Kishindo Uchaguzi Kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema na Kuwa Mwenyekiti Rasmi wa Bawacha

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Halima Mdee akizungumza na wajumbe wa mkutano huo baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Bawacha.

 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kulia) akipongezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo (Bara), Hawa Mwaifunga.

 Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema wakiwa katika mkutano huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga akilia kwa furaha baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika juzi.

 Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah.

Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), wakifungua shampeni kusherehekea ushindi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.Picha na Francis Dande