Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika kata ya Mponde, akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Septemba 29, 2014.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Kijiji cha Mponde, Kinana ameitaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kiwanda cha Chai cha Mponde, kufa baada ya kubinafsishwa kwa njia zinazoashiria kutofuata utaratibu unaotakiwa.
Pia Kinana ameahidi kulifikisha suala hilo katika vikao vikubwa ikiwemo cha Kamati Kuu ya CCM, ili kuhakikisha unapatikana ufumbuzi wa kero hiyo ikiwemo kuwachukulia hatua viongozi waliohusika.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili katika kijiji cha Mbuzii kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata ya Mbuzii, katika jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, leo Septemba 29, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadili kwa makini jambo na Mbunge wa Bumbuli, Waziri Januari Makamba, wakati wa kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mbuzii, jimboni humo, leo, Septemba 29, 2014.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA