Monday, September 01, 2014

KAMPUNI YA TRAVELPORT YAZINDUA MFUMO MPYA UTAKAOWAWEZESHA MAWAKALA WA NDEGE KUUZA TIKETI KIURAHISI ZAIDI



KAMPUNI YA TRAVELPORT YAZINDUA MFUMO MPYA UTAKAOWAWEZESHA MAWAKALA WA NDEGE KUUZA TIKETI KIURAHISI ZAIDI
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky utakaotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents)  uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua ramsi mfumo huo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo huo mpya utakaotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents)  uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha (wa pili kushoto) akifurahi pamoja na Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw (kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Galileo Tanzania,Mwalim Ally wakati wa kupongezana baada ya kuzindua mfumo huo mpya.
Meneja wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege kutoka Kampuni ya Travelpotr,Gloria Urassa akiwasilisha mada ya namna kutumia huduma hiyo itakayotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents) wakati wa hafla uzinduzi wake uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
Meneja wa Ufundi kwa Kampuni ya Travelport Tanzania,Julius Haule akitoa maelezo ya namna mfumo huo wa Pricese Sky unavyoweza kuwarahisishia Mawakala wa kuuza tiketi za ndege kuuza tiketi hizo za mashirika yote ya ndege ya ndani ya nchi ambazo hapo awali zilikuwa hazitumii mfumo huo.
Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani kwa niaba ya mawakala wa tiketi za ndege nchini kwa kufanikishiwa mfumo huo.