Monday, September 01, 2014

Wabunge Afrika Mashariki watembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)




Wabunge Afrika Mashariki watembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto)  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.