Monday, September 01, 2014

BODI YA WAKURUNGENZI YA DAWASA YATEMBELEA ENEO LA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA



BODI YA WAKURUNGENZI YA DAWASA YATEMBELEA ENEO LA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA
Meneja Usimamizi, Undeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaama (DAWASA), Bi.Modesta Mushi akiwaneosha Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi wa mamlaka hiyo ramani ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, Agosti 29, 2014 wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), kuhusiana kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda litakaloweza kutoa huduma kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Archard Mtalemwa akisisitiza jambo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Alhaji Said El-Maamry (kulia), akimuuliza swali Mhandisi. John Kirecha kuhusiana fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi huo, likiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa huo.
Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi hao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI