Friday, August 01, 2014

UCHAGUZI DMV: Mgombea wa Nafasi ya makamo wa Rais,Salima Moshi anadi sera zake




UCHAGUZI DMV: Mgombea wa Nafasi ya makamo wa Rais,Salima Moshi anadi sera zake
Mimi Salima Moshi,Mgombea wa Nafasi ya makamo wa Rais DMV,
Napenda kuwa hakikishia kuwa tutakuwa bega kwa bega,tutashirikiana kwa pamoja ili kuendeleza Jumuia yetu hapa DMV.

SITOJITOA kamwe katika dhamana mtakayonikabidhi kama ilivyotokea kwa mgombea mwenzangu tarehe 18 July alijitoa Ubalozini mbele ya viongozi na kusema anajitoa hawezi kugombea tena na kuniendorse mimi.

 Hivyo mtu akijitoa Hataki lawama ina maana kazi haiwezi Msije mkamlaumu,tumeshuhudia wagombea aina hii,hatutaki kufanya makosa.

  Nichagueni mimi,Najiamini Ni mchapa kazi,Nina uwezo wa kuongoza ni Mwadilifu na niko tayari kujitolea wakati wowote Kwa heshima na Taadhima.

Naomba Kura zenu