Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ummy Ali Mwalimu akimkabidhi kadi ya hongera mtumishi wa Bunge hilo, Mhe. Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania. Awali Mhe. Mgonya alikuwa ni Msaidizi wa Waziri Mkuu.
Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Ummy Ali Mwalimu akimlisha keki mtumishi wa Bunge hilo, Mhe Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. William Lukuvi , akimlisha keki mtumishi wa Bunge hilo, Leila Mgonya katika shehere ya kumwuaga baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania. Picha na Kamati ya Bunge Maalum la Katiba