Friday, August 15, 2014

MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI



MISS ILALA 2013 DORICE MOLLEL ATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA UMEME WA GESI NA KUTUNZA MAZAO RIELA NCHINI UJERUMANI
photo
Bw. Karl Heinz Knoop akielezea historia fupi kuhusu kampuni yake kwa wanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu  Nyerere akiwemo Miss Ilala 2013 Dorice Mollel wanaoshiriki program ya mwezi mmoja nchini Ujerumani.

Miss Ilala 2013 Dorice Mollel (kushoto pichani) akiwa kwenye program ya mwezi mmoja, na wenzake 8 kutoka Chuo cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere ambapo wamepata nafasi ya kwenda kutembelea Kiwanda cha Kilimo kilichoanzishwa mwaka 1972 ambacho kinamilikiwa na Bw. Karl Heinz Knoop , mwenye uzoefu wa miaka 50 ambaye anatarajia kujenga kiwanda hiki pia nchini Tanzania mkoani Kilimanjaro Moshi kitakachofahamika kwa jina la Reila amabavyo pia vipo zaidi ya nchi 11 duniani na kwa Afrika ni Tanzania pekee tumepata bahati hiyo ya kuletewa Teknlolojia anayotumia ya kutengeneza umeme wa gesi na pia kutunza mazao, hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo Tanzania.
Dorice Mollel amesema " hichi ni kitu cha muhimu sana nikiwa kama mrembo nikirudi nyumbani na kuieleza jamii inayonizunguka ili kutuletee faida baadae nchini kwetu".
photo (1)