Sunday, August 24, 2014

MSHAMBULIAJI WA CAMEROON AFARIKI BAADA YA KUPIGWA KICHWANI NA KITU KILICHORUSHWA NA MASHABIKI UWANJANI


MSHAMBULIAJI WA CAMEROON AFARIKI BAADA YA KUPIGWA KICHWANI NA KITU KILICHORUSHWA NA MASHABIKI UWANJANI

Tragedy: Cameroonian striker Albert Ebosse died                  after being hit in the head by object thrown from                  stands

MCHEZAJI mmoja wa soka raia wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya Algeria.

Kwa mujibu wa BBC, mshambuliaji huyo (pichani kulia) mwenye umri wa miaka 24 Albert Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.

Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo.