Hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha lumuma Mpwapwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki ilitanguliwa na ibada takatifu iliyoongozwa na makamu wa askofu kanisa katoliki dodoma padiri Chesco Msaga (wa pili kulia) kituo hiko cha afya kinamilikiwa na kanisa hilo kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akiwa amembeba mtoto aliyepewa jina la Rehema na mama yake kama ishara ya kumuenzi mkuu huyo wa Mkoa kwa kuwa mtoto huyo alizaliwa kwenye kituo cha afya lumuma mpwapwa majira ambayo mkuu huyo wa Mkoa alikuwa ndio anawasili kituoni hapo kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD lililogharimu kiasi cha Milioni 350 mwishoni mwa wiki.
Picha ya pamoja kati ya mkuu wa mkoa dodoma, viongozi wa kanisa katoliki na shirika la watawa la Mt. Gema dodoma na marafiki wa lumuma raia kutoka italia waliofadhili ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya lumuma mpwapwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo hilo mwishoni mwa wiki.
Umati wa wananchi wa kata ya lumuma mpwapwa na maeneo ya jirani ya wilaya ya kilosa morogoro waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha kata ya lumuma mpwapwa mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akikata utepe kufungua jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha Lumuma Mpwapwa mwishoni mwa wiki, kushoto ni mkuu wa wilya ya mpwapwa Christopher Kangoye na kulia ni bw. Anjelo Dauria mwenyekiti wa shirika la marafikii wa lumuma la Italia waliofadhili Milioni 350 za ujenzi wa jengo hilo, kituo cha Lumuma Mpwapwa kinamilikiwa na Kanisa katoliki dodoma kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema.
Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi akifungua kitambaa kuashiria ufunguzi wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya Lumuma mpwapwa mwishoni mwa wiki, jengo hilo lina thamani ya Milioni 350, kjituo hiko cha afya kinamilikiwa na kanisa katoliki dodoma kupitia shirika lake la watawa la Mt. Gema, kushoto ni mkuu wa shirika hilo Sr. Florencia Mbeyu.
Muonekano wa jengo la huduma kwa wagonjwa wa nje OPD kwenye kituo cha afya cha lumuma Mpwapwa lililogharimu milioni 350 kwa ufadhili wa shirika la marafikii wa lumuma la Italia, jengo hilo lina idara zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya wagonjwa wa nje, lilifunguliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa Dodoma Dr Rehema Nchimbi.