Monday, August 11, 2014

MASHIRIKA MBALIMBALI YAOMBWA KUDHAMINI PIA MATAMASHA YA MUZIKI WA INJILI




MASHIRIKA MBALIMBALI YAOMBWA KUDHAMINI PIA MATAMASHA YA MUZIKI WA INJILI
1
Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba. 

 Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilisha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba,Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo wa ramadhan.

'' kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia kupunguza gharama za uandaaji, jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii'',alisema Mabula.
01
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
6
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo. 
2
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.