Thursday, July 17, 2014

Waziri Membe azungumza na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha St. Thomas cha Marekani



Waziri Membe azungumza na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha St. Thomas cha Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na kiongozi wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha St. Thomas, Fr. Jean-Piere Bongilo kilichopo  Minessota nchini Marekani waliofika Wizarani kumsalimia. Chuo cha St. Thomas kilimtunuku Shahada ya Uzamivu wa Heshima, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2006.
Baadhi ya Wanafunzi hao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Balozi Joseph Sokoine (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kushoto) na baadhi ya wanafunzi hao.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na wanafunzi hao.
Picha na Reginald Philip