Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akipokelewa kwa shangwe na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kipara-Mtua, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kabla ya kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo na kujua kero mbalimbali zinazowakabili viongozi hao. Aidha, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akikitunza kikundi cha kwaya cha CCM Kata ya Kipara-Mtua baada ya kutumbuiza katika mkutano wake na Viongozi wa Kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kipara-Mtua, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (meza kuu katikati) akimsikiliza kwa makini Mkandarasi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Rabinarayan Bishoyi (kulia) wakati alipokuwa anatoa maelezo kwa viongozi wa CCM Kata ya Mtua (hawapo pichani). Kwa mujibu wa Mkandarasi huyo, tayari ameanza kuweka nguzo za umeme kutoka Nachingwea mjini kwenda vijiji vya Namatula, Kihuwe, Naipingo, Mapwechero, Farm 15, Kipara Mtua, Jiungeni na Mtua ambapo vijijini hivyo vinatarajiwa kupata umeme hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco, Josiah Hegeleize ambaye Shirika lake linashirikiana na REA kuleta umeme katika vijiji hivyo.
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto hajavaa kofia), kwa kuandaa futari maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti Mkuu wa Nachingwea, mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa ajili ya kutoa sadaka kwa waumini hao katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Picha zote na Felix Mwagara.