Wednesday, July 23, 2014

Matumizi ya Magogo viwandani marufuku - Waziri Mahenge



Matumizi ya Magogo viwandani marufuku - Waziri Mahenge
 Wawekezaji wote Nchini wanatakiwa kuhakikisha wanaacha kutumia magogo katika uzalishaji badala yake watumie tekinolojia ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya tabia ya nchi na uchafuzi wa Mazingira yanayotokana na ukataji miti. 
 Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt. Injinia Binilith Mahenge wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni na mafuta ya kupikia (BIDCO) kilichopo mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 Amekiagiza kiwanda hicho kuacha mara moja matumizi ya magogo kwani inaathari kubwa sana kwa jamii. Hata hivyo amesema kuwa atatembelea tena kuangalia kama wameacha kutumia magogo ndani ya miezi sita, endapo watabainika wanaendelea kutumia magogo,hatua kali itachukuliwa juu ya Kiwanda hicho endapo watakiuka masharti waliyopewa.Amesema Kiwanda kitafungwa mara moja. 
 Hata hivyo Mh. Mahenge amewaomba wawekezaji wa viwanda vingine kuiga mfano wa kiwanda cha Coca Cola katika utunzaji wa Mazingira, kwani wao ni mfano mzuri kwa viwanda vingine kwa kuanzisha technolojia nyengine ya kuchunguza maji taka kama ni salama kwa viumbe hai. 
 Amemalizia kwa kusema "Tunapenda wawekezaji lakini ni wale wanaotunza na kuyaenzi mazingira kwa usalama wa wananchi na nchi yetu kwa ujumla".
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano  Mahenge ( wa pili kulia)  pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu (wa kwanza kushoto), wakiwa katika ziara  fupi ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha Coca Cola kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. Wakiwa pamoja na mkurugenzi wa uzalishaji soda katika kiwanda hicho Bw. Louis Coetzee (wa kwanza kulia).
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uzalishaji soda Bw. Louis Coetzee ( wa kwanza kulia), akielezea jinsi kiwanda hicho kinavyotumia maji taka kulinda Mazingira ya kiwanda.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Dkt. Injinia Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake na kuwaambia kwamba nchi inahitaji wawekezaji wanaotunza na kulinda Mazingira yetu. Viwanda alivyovitembelea ni kiwanda cha kuzalisha Mafuta ya kula na sabuni (BIDCO), M.M.I steel mill kinachozalisha Nondo na Mabati pamoja na kiwanda cha Coca Cola vilivyopo Mikocheni  jijini Dar es Salaam.