Sunday, July 20, 2014

MABOMU YA MACHOZI YALAZIMIKA KUTUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI WALIOVAMIA NA KUANZA KUCHOTA MAFUTA KWENYE LORI LA MAFUTA BAADA YA KUPATA AJALI MKOANI IRINGA




MABOMU YA MACHOZI YALAZIMIKA KUTUMIKA KUWATAWANYA WANANCHI WALIOVAMIA NA KUANZA KUCHOTA MAFUTA KWENYE LORI LA MAFUTA BAADA YA KUPATA AJALI MKOANI IRINGA

Jeshi la polisi mkoani Iringa limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi ambao walivamia na kuanza kuchota mafuta kwenye lori la kubeba mafuta baada ya kupata ajali. 

 
Ajali hiyo imetokea jana eneo la msitu wa serikali wa Saohil wilayani Mufindi kwenye barabara kuu ya Iringa –Mbeya ambapo watu wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
 
Polisi wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiendelea kumiminika kutaka kuiba mafuta kwenye lori hilo ili kuwaepusha na hatari ambayo ingeweza kutokea kama lori hilo lingeshika moto.
 
Mashuhuda wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya lori la mizigo lililokuwa linatokea mkoani Mbeya na hivyo kukosa mwelekeo na kuligonga gari la kubeba mafuta lililokuwa linatokea mkoani Iringa na kuanguka.
 
Jeshi la polisi mkoani iringa limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.