Friday, July 04, 2014

JKT Wakanusha kutokea vifo Katika Mafunzo Kutokana na Ukatili na Mazoezi Makali



JKT Wakanusha kutokea vifo Katika Mafunzo Kutokana na Ukatili na Mazoezi Makali
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekanusha taarifa zinazosambazwa kupitia simu na mitandao ya kijamii kuwa vijana watatu wamefariki baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili katika mafunzo yanayoendelea kwenye kambi ya JKT Oljoro, Arusha.

Msemaji wa JKT, Luteni Kanali Erick Komba, alikanusha taarifa zinazoenezwa juu ya kuhusika kwa jeshi hilo na vifo hivyo kikiwamo kifo cha mwanamke aliyefariki katika kambi hiyo.

Kanali Komba alisema kumezuka taarifa zenye nia ya kulichafua JKT na kupotosha jamii baada ya kifo cha Honorata aliyefariki kwa upungufu wa damu (anaemia).

"Taarifa zilizosambazwa ni uzushi, hakuna vifo vya vijana watatu vilivyotokana na ukatili katika kambi ya JKT Oljoro. Ukweli ni kwamba amefariki kijana mmoja anayeitwa Honorata Oiso," Kanali Komba aliwaambia waandishi wa habari jana.

"Kuna mtu anayetumia kifo hiki kusambaza ujumbe wa uongo kwa jamii. Wazazi wake wamethibitisha ukweli juu ya kifo cha mtoto wao," aliongeza.

Source: Nipashe News Paper