Sarafu ya Shilingi Mia Tano ambayo Benki Kuu ya Tanzania inatarajia kuitoa hivi karibuni. Noti ya Mia Tano maarufu kama 'Jelo' itaendelea kutumika, ila itaondolewa taratibu katika mzunguko, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki na Sarafu wa BoT, Bw Emmanuel Boaz, aliyeiambia Globu ya Jamii kwenye banda la Benki Kuu katika Maonesho ya SabaSaba jijini Dar es salaam.