Thursday, July 17, 2014

HAFLA YA THT JIJINI DAR


HAFLA YA THT JIJINI DAR
 Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo  wanahabari,wadau na wasanii wa filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo wanaanza kumsimamia msanii huyo pamoja na kazi zake.Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba
 Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akiongea katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo wanaanza kumsimamia msanii huyo pamoja na kazi zake.
 Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akimkabidhi cheti cha heshima msanii wa kizazi kipya,Mwasiti kwa kuwa msanii mwenye nidhamu kubwa kutoka chuo cha kipaji cha THT kwa muda mrefu.
Mmoja wa Maprodyuza mahiri kutoka THT ajulikanae kwa jina la kisanii Imma ze Boy akikabidhiwa cheti chake cha kuwa kijana anaejituma kwa moyo moja katika suala zima la utendaji kazi ndani ya kituo cha THT.
Vyeti vya heshima vilikwenda na hata kwa vijana wanaochipukia ndani ya THT
Msanii Lameck Ditto akipokea cheti chake cha heshima (kijana mwenye nidhamu ndaniya kituo cha THT) kutoka kwa Mkurugenzi wa THT,Ruge Mutahaba,
MKurugenzi wa Kampuni ya NO FAKE ZONE,Abby akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari,wadau na wasanii wa filamu na muziki,katika hafla ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014  ambaye anahamia hiyo,itakayokuwa ikisimamia kazi zake za msanii huyo.Linah pia alizindua video yake mpya chini ya kampuni NFZ iitwayo OLe Themba.





Kicheko kidogo mbele ya camera ya Globu ya jamii
Mwenyekiti wa Bongomuvi Steve Nyerere akizungumza  jambo na Wadau wa Muziki
Wasanii na Wadau wa muziki wakifuatilia uzinduzi wa video mpya ya Msanii Linah 
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa vido mya ya Linah iitwayo OLe Themba
Msanii Linah akiwa amepozi kwenye bango lake linaloelezea ujio wa video yake mpya ya Ole Themba pamoja na jina la kampuni anayohamia
Wadau wa Muziki sambambana Wanamuziki walikuwepo kushuhudia tukio hilo likiwemo la uzindui wa vieo mpya ya msaani Linah
Baadhi ya wanahabari waliokuwa wakirekodi tukio hilo adhimu 
Wageni waalikwa wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa video mpya ya Msanii Linah iitwayo Ole Themba
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.