Saturday, July 05, 2014

FIFA YAIPA NIGERIA SIKU TATU

 
 
 
 
Victor Moses wa NIgeria katika Kombe la Dunia akivutana na Yohan Cabaye wa Ufaransa

Shirikisho la Kandanda la Dunia, FIFA, limeionya Nigeria kwamba itatolewa katika kandanda ya kimataifa iwapo serikali haitalirejesha tena shirika la kandanda la Nigeria, Nigerian Football Federation, ifikapo Jumaane juma lijalo.
Siku ya Alkhamisi serikali iliifuta Nigerian Football Federation na Ijumaa rais wa shirika hilo alikamatwa baada ya kurudi kutoka Kombe la Dunia.
Nigeria ilishindwa kwenye mechi na Ufaransa na hivo kukosa kuingia katika robo-fainali.
FIFA imesema imetiwa wasi-wasi na hatua ya serikali ya Nigeria dhidi ya chama cha kandanda cha nchi hiyo.
Kanuni za FIFA zinaeleza wazi kuwa wanachama wake lazima waruhusiwe kufanya kazi yao bila ya kuingiliwa kati na serikali.
Wakuu wa Nigeria wamekifuta chama cha kandanda cha taifa na piya kumkamata rais wa chama; na waziri wa michezo amemteua mkurugenzi wake kuongoza chama hicho.
Haijulikani sababu ya serikali ya Nigeria kufanya hivyo.
Lakini iwapo serikali haitabadili uamuzi wake basi Nigeria haitaweza kushiriki katika mechi za kimataifa, mazoezi na kadhalika.Chanzo BBC SwahilI