Tuesday, July 01, 2014

Daktari na Mgonjwa wa Meno wafumaniwa wakijiandaa kufanya Mapenzi ndani ya Hospitali moja Temeke jijini Dar ....Mgonjwa alikuwa ameshavua nguo, Alijihimu kung'olewa Jino


Daktari na Mgonjwa wa Meno wafumaniwa wakijiandaa kufanya Mapenzi ndani ya Hospitali moja Temeke jijini Dar ....Mgonjwa alikuwa ameshavua nguo, Alijihimu kung'olewa Jino

Daktari wa meno aliyejulikana kwa jina la Dokta Ngariba (54), amejikuta ndani ya janga la tuhuma za ngono baada ya wapiga picha za Udaku kunasa sakata lake na mwanamke aliyedai ni mgonjwa wa jino aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamida (20).
 
Tukio hilo la kushangaza lilijiri Juni 9, mwaka huu ndani ya Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Temeke kilichopo Kigamboni jijini Dar ambapo timbwili hilo lilitokea.


Ilikuwa wakati mwandishi  akizunguka katika Jiji la Dar es Salaam  kusaka matukio ndipo alipopita nje ya kituo hicho alisikia sekeseke kutokea kwenye chumba ambacho baadaye kilibainika na cha kung'olea meno.
 
Katika uchunguzi na ufuatiliaji , mgonjwa huyo alisikika akidai kwa polisi waliofika kutuliza sakata kuwa, alijihimu kwenye kituo hicho kwa lengo la kung'oa jino lakini katika hali ambayo hakuitarajia daktari huyo alimtaka kimapenzi naye akajikuta akitumbukia.
 
"Mimi nimekuja kung'oa jino, linaniuma leo sijui siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka kimapenzi. Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria," alisema mwanamke huyo ambaye alikutwa ameshavua dera.

Daktari akijitetea.....

Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha mgonjwa wake huyo atambe kiasi hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa, alimpokea mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha kung'olea meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha kumvua na yeye shati na baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.
 
Akiendelea kuzungumza mbele ya Polisi wa Kituo cha Kigamboni waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha matibabu ya meno, daktari huyo alisema:
 
"Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua ni mgonjwa anataka tiba ya kung'olewa jino. 
 
"Sasa nikiwa katika maandalizi ghafla nikamwona anavua nguo na kisha akanivaa mimi na kuanza kunivua shati. Nashangaa sana anaposema nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani."
 
Baada ya maelezo ya Dokta Ngariba, mwandishi  alikuwa na maswali yake lakini hakupewa nafasi ya kuyauliza kwa vile alidandia ugomvi.
 
Swali la kwanza; kama kweli Dokta Ngariba alivamiwa na kuvuliwa nguo na mgonjwa huyo, alipiga kelele kuomba msaada kutoka kwa watumishi wenzake?
 
Swali la pili; mpaka mgonjwa anajivua nguo zake kisha kumvua yeye shati na baadaye kuelekea kwenye fraizi ya suruali, yeye alikuwa anawaza nini akizingatia ni mgonjwa wa meno?  
 
Wakielekea kituo cha Polisi Kigamboni.

Uwazi lilizungumza na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sylvia Mamkwe kuhusu sakata hilo ambapo alisema:
 
"Taarifa hizo nazisikia kwako, niko safarini, nitafuatilia. Kama ni kweli hatua zinachukuliwa kwa waajiri wake ambapo najua kwa kosa kama hilo ni kupoteza kazi."