Tuesday, July 01, 2014

PPF WAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WAKATI KATIKA MAONYESHO YA 38 YA SABASABA




PPF WAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WAKATI KATIKA MAONYESHO YA 38 YA SABASABA
 Afisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Jackline Jackson akitoa ufafanuzi juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa wateja waliotembelea Banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Kufanyika katika viwanja hivyo.
 Afisa Rasilimali Watu, Utawala na Ushauri wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Happiness Mmbando (Kulia) akimuhudumia mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Katika Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar Es Salaam. 
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar Es Salaam
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya Pamoja na Mmiliki wa Mtandao wa Michuzi, Ndg Muhidin Issa Michuzi(mwenye suti nyeusi) mara baada ya kukabidhiwa zawadi na PPF wakati alipotembelea Banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba.
Mwandishi wa Habari mkongwe, Ndg Abdallah Majura (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko na Pensheni wa PPF pamoja na Mdau wa habari wakati walipotembelea banda la PPF katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog