
Mkate uliotayari kwa kuliwa ooohhh asikwambie mtu saafi sana!
Chef Issa anashukuru Allah kupata bahati ya kualikwa na chama cha scout kwenda kuwafundisha vijana mbinu za mapishi wakiwa porini. Dah! waliipenda na kufagilia sana walitengeneza mkate wa kubanika kwa kutumia mti na moto wa kuni.

Kundi la vijana wa scout na uongozi wao hapa ni baada ya kuwasha moto tukisubiri upungue na kuni zote zishike moto tuanze kubanika mkate.

Chef Issa (kulia) akiwa na vijana wa scout

Huu ndio mkate wenyewe ukiwa unaelekea kuiva

Baada ya moto kupungua na magogo kuwaka kama mkaa hapo sasa safi unaweza endelea kubanika mkate wako hakikisha fimbo ni ndefu ili usiungue mikono.