Tuesday, July 01, 2014

BENKI YA CRDB YABORESHA HUDUMA ZA SIMBANKING




BENKI YA CRDB YABORESHA HUDUMA ZA SIMBANKING
MkurugenziMtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kuboreshwa kwa huduma za Benki hiyo kupitia simu za kiganjani "Simbanking".
MkurugenziMtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (katikati), akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Esther Kitoka wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuboreshwa kwa huduma za Benki hiyo kupitia simu za kiganjani "Simbanking".
Meneja wa Benki ya CRDB anayeshughulikia Huduma za Kibenki kwa Njia ya Mtandao, Mangire Kibanda akitoa mada kuhuu huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo ikiwemo huduma za kuhamisha fedha kutoka katika akaunti moja kwenda katika akaunti nyingine kupitia simu ya kiganjani "Simbanking"
Mkurugenzi wa kuzuia vihatarishi CRDB, James Mabula akitoa mada kuhusu usalama katika kufanya miamala.

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuleta ubunifu wa kisasa na kiteknolojia Benki ya CRDB imezidi kuboredha huduma yake ya 'simbanking' ambayo utolewa kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha huduma mpya ya kufanya miamala popote alipo mteja. 

Akizingumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei alisema, ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania anaikubali na kuipokea huduma hiyo, benki yake imerahisisha namna ya kujiunga na kujisajili. 

Alisema kila mteja atapata fursa ya kujiunga yeye mwenyewe bila kuhitaji kutembelea matawi yao wala kujaza fomu ya aina yoyote hile. "Huduma ya 'simbanking' ina faida nyingi sana kwani ni sawa na kubeba akaunti yako popote ulipo na kuweza kuifikia kiurahisi yaani ni sawa na kutembea na benki yako kila uendako, ieleweke kuwa kujiunga ni rahisi sana, mteja atatakiwa kupiga namba *150*03# katika simu yake ya mkononi na kufuata maelekezo rahisi," alisema. 

 Kimei amewataka wateja wa benki hiyo kuendelea kutunza taarifa zao vizuri kwani wameibuka matapeli katika mitandao ya kijamii wanaojaribu kuwalaghai wateja hao kwa kuwaomba taarifa za akaunti zao. 

"Jambo la msingi hapa nikuendelea kuwasisitiza wateja wetu juu ya umuhimu wa kutunza vizuri taarifa za akaunti zao ikiwemo kadi na namba za siri ili wajiepushe na matapeli hao," alisema. 

Mkurugenzi wa kuzuia vihatarishi CRDB James Mabula alisema, wao kama benki wanawashauri wateja wao pale wanapokuwa wakifanya miamala na kuhisi kuwa kuna mtu nyuma wasifanye kwasababu mtu huyo anaweza kuiba taarifa muhimu. Pia Mabula aliwataka wateja kuepuka kutumia namba za siri ambazo ni rahisi, miaka ya kuzaliwa au zinazofuatana kwani ni rahisi kwa mtu mwingine kuweza kuzibuni.