WAWAKILISHI pekee wa bara la Afrika waliokuwa wamesalia kwenye michuano ya Kombe la Dunia – Nigeria na Algeria – wameaga rasmi michuano hiyo katika hatua ya raundi ya pili baada ya kuchukua vipogo kutoka kwa wawakilishi wa bara la Ulaya, Ufaransa na Ujerumani.
Nigeria waliocheza na Ufaransa walikukuruka hadi dakika 78 na kujikuta wakikubali bao rahisi lililofungwa na kiungo wa Juventus Paul Pobga kabla hawapokea bao la pili kwa njia ya kujifunga kupitia kwa beki wake Yobo katika dakika za majeruhi (90+2).
Algeria waliocheza na Ujerumani walibana na kulazimisha sare ya 0-0 katika dakika 90 za kawada na kufanya mchezo uende hatua ya dakika 30 za 'extra time' ndipo waliposalimu amri na kuruhusu bao 2-1.
Bao la kwanza lilifungwa na mchezaji wa Chelsea Andre Schuerrle dakika ya pili tu ndani ya dakika 30 za nyongeza na ilipotimu dakika ya 120 Ozil akaifungia Ujerumani bao la pili baada ya piga nikupige.
Sekunde chache baadae, Algeria wakafunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Abdelmoumene Djabou.
Kwa matokeo hayo, Ujerumani sasa itaumana na Ufaransa katika hatua ya robo fainali Julai 4.