Wednesday, June 11, 2014

WAKENYA WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA,NI WALE WALIPORA FEDHA BENKI YA NMB TAWI LA MWANGA.




Breaking Newss:WAKENYA WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA,NI WALE WALIPORA FEDHA BENKI YA NMB TAWI LA MWANGA.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAHAKAMA kuu kanda ya Moshi imetoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa wawili raia wa Kenya katika  kesi ya mauaji ya askari Polisi, Pc Michael Milanzi, wakati wa tukio la uporaji  wa fedha katika benki ya NMB tawi la Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Mbali na hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu, Kakusulo Sambo kwa zaidi ya saa, nne ,Mshatakiwa wa tatu katika kesi hiyo ,Karisti Kanje(Mtanzania) yeye amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitano(5) jela kwa kosa la kuhifadhi na kutorosha watuhumiwa wa mauaji ya askari polisi.