Kampuni ya mawasiliano                nchini ya Vodacom imendelea na azma yake ya kuhakikisha                inawafaidisha wateja wake kupitia huduma zake huku                wakitengeneza nafasi za ajira kupitia maduka yake                yanayoendelea kufunguliwa nchi nzima. 
         Hayo yameelezwa na Mkuu                wa Idara ya Mauzo ya Rejareja, Upendo Richard wakati                akizindua duka jipya la Vodacom maeneo ya Sinza Afrika                Sana ambalo linakuwa ni la 18 kwa wilaya ya Kinondoni                pekee na la 79 Tanzania nzima. 
         "Dhamira kubwa ya                kusambaza maduka haya ni kusogeza na kuboresha huduma kwa                wateja wetu popote walipo lakini pia tunawatengeneza                watanzania nafasi za ajira. Ajira hizi kwa namna moja au                nyinigine ni suluhu la upungufu wake nchini na pia                hupunguza mzigo kwa serikali katika jitihada za                kuhakikisha watu wanajiajiri wenyewe." Alisema Bi.                Richard 
         Ameendelea kuwa kwa                kila duka la Vodacom linalofunguliwa, watu watano mpaka                saba huajiri kwa nafasi kama vile za; meneja wa duka,                uhasibu, wauzaji simu, watoaji ushauri kwa wateja pamoja                na wakala wa M-Pesa. 
        Amesema kuwa duka hili                likiwa ni la 79 kufunguliwa nchi nzima, takwimu                zinaonyesha kuwa kuna takribani idadi ya wafanyakazi zaidi                ya 400 wanafanya kazi katika maduka yote ya Vodacom                yaliyosambaa nchi nzima. 
         "Wateja wote wa Vodacom                sasa wasipate tabu za kwenda maeneo ya mbali kutafuta                huduma za kimawasiliano badala yake watumie duka hili                lililopo hapa Sinza Afrika Sana." Alisema Bi. Richard na                kuongezea, "Huduma zinazotolewa hapa ni sawa na maduka                mengine ili kuweza kutimiza haja zao na kuepukana na                usumbufu wa kwenda maeneo kama Mlimani City, Quality                Center. Mkifanya hivyo mtasababisha msongamano wa watu                hali ambayo inapelekea na foleni ambazo zinasababisha                kuchelewa kupata huduma." 
         Nae mteja wa kwanza                kutumia duka hilo mara baada ya kufunguliwa rasmi, Alfred                Joseph, ambaye ni mkazi wa Sinza Afrika Sana ameishukuru                Vodacom kwa jitihada zao za kusogeza huduma kwa wateja na                kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri umbali mrefu. 
         "Kabla ya kufunguliwa                kwa duka hili, tulizoea kwenda Mlimani City kufuata huduma                ambapo ilikua ni changamoto kubwa sana. Kwa mfano kwetu                sisi wafanyakazi, muda mwingine unakuwa umetoka kazini                umechoka halafu unahitaji huduma kwa uharaka lakini                unashindwa kuzifikia mpaka uanze safari ya kwenda Mlimani                City. Kwa kweli ulikua ni usumbufu mkubwa sana,                tunashukuru kwa kuliona hilo na kulifanyia kazi na sidhani                kama nitasumbuka tena kwenda huko." Alisema mkazi huyo 
         Akitoa machache wakati                wa uzinduzi Meneja wa duka hilo, Swaum Manengelo                amebainisha shukrani zake za dhati kwa Vodacom kwa                ushirikiano waliouonesha mpaka duka hilo linakamilika na                kuanza kutoa huduma kwa wateja. 
         "Naweza kusema ndoto ya                wakazi wa Sinza Afrika Sana kuwa na huduma za Vodacom                karibu yao zimetimia, ufunguzi wa duka hili ni ushahidi                tosha. Ningependa kuwakaribisha wateja wote wa kutoka                maeneo haya na ya jirani kutembelea dukani hapa na                kuhudumiwa." Alisema Bi. Manengelo, na kumalizia,                "Ningependa kuwatoa hofu wateja wetu wasihofie ubora wa                huduma na bidhaa zinazopatikana hapa kwani wengi hudhani                labda huduma zinazotolewa Mlimani City au Quality Centre                ni bora zaidi, hilo si kweli na nathubutu waje kujaribu                leo." 
                 Meneja                  wa duka jipya                  la huduma kwa wateja la                  Vodacom lililopo Sinza                  Afrika Sana jijini Dar es Salaam, Swaum Manengelo                  akifungua mlango kuashiria ufunguzi rasmi wa duka hilo.                  Wakishuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Idara ya Mauzo ya                  Rejareja Upendo Ricahrd (kushoto)                  na Meneja Uhusiano wa Nje  wa                  kampuni hiyo Salum                  Mwalim (kulia).
                 Mkuu                  wa Idara Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania, Upendo Richard  akikagua huduma                  na bidhaa mbali mbali  ndani                  ya duka jipya la huduma kwa wateja lililopo Sina Afrika                  Sana jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya                  kuzinduliwa rasmi hivi karibuni. Hilo ni duka la 18 la                  huduma kwa wateja Wilayani Kinondoni na la 79 nchi                  nzima.
                Mkuu                  wa Idara ya Mauzo ya Rejareja wa kampuni ya Vodacom                  Tanzania, Upendo Richard (kushoto) akimkabidhi                  Meneja wa duka  jipya                  la hudfuma kwa wateja la                  Vodacom Sinza Afrika Sana Swaum                  Manengelo funguo                  ya duka hilo kuashiria                  ufunguzi rasmi wa duka hilo kuanza                  kutoa huduma kwa wateja  Akishuhudia                  tukio hilo katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni                  hiyo, Salum Mwalim.Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni                  jijini Dar es salaam.
        


 
