Thursday, June 12, 2014

UPASUAJI WA MATOBO LAPAROSCOPIA WAFANYIKA LIVE KAIRUKI HOSPITALI


UPASUAJI WA MATOBO LAPAROSCOPIA WAFANYIKA LIVE KAIRUKI HOSPITALI
 Daktari Bingwa wa upasuaji Dk. Muganyizi Kairuki akizungumza wakati wa semina ya upasuaji kwa njia  matobo Laparoscopia uliofanyika LIVE katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliwashirikisha madakatari wa ndani na nje ya nchi.
 Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka Afrka Kusini, Prof. Zacharia Koto (wa pili kulia), akisaidiana na daktari bingwa wa upasuaji kutoka Namibia Dk. S. Kaikai (kulia) na Dk. Muganyizi Kairuki wakimfanyia operesheni ya kuondoa mawe tumboni mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki, wakati wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo iliyofanyika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Madaktari wakiwa kazini.
 Madaktari wakishauriana jambo wakati wa operesheni.
 Madktari wakiwa kazini.
 Dk. Sunil Popat kutoka India akifanya operesheni ya matobo Laparoscopia Live.
 Kutoka kushoto ni Dk. Ali Mwanga wa Muhimbili, Dk. Steven Mbata wa Kairuki Hospitali, Dk. Brown Ndofor wa Namibia Dk. Sunil Popat wa India na Sister Salvata Kulaya wa Kairuki Hospitali.
 Chumba cha upasuaji kikiwa na vifaa vya kisasa.
  Kutoka kushoto ni Dk. Jerome Mtiramweni wa HKMU, Dk. Brown Dafor wa Namibia, Dk. Sunil Popat wa India na Sister Salvata Kulaya wa Kairuki Hospitali.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni, akizungumza wakati wa semina ya upasuaji wa matobo Laparoscopia uliofanyika LIVE katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 Dk. Muganyizi Kairuki (kushoto) akiwaonyesha madaktari vifaa vinavyotumika wakati wa kufanyia operesheni ya matobo Laparoscopia, madaktari waliohudhuria kwa mafunzo vitendo namna ya kutumia vifaa hivyo.  
Professa Esther Mwaikambo akichangia mada wakati wa semina hiyo.
 Professa Zacharia Koto (kushoto), akipokea ngao kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni
 Dk. Paul Kisanga wa Selian Hospitali Arusha, akipokea cheti kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni.
Baadhi ya madaktari wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya washiriki wa semina ya upasuaji kwa njia ya matobo kwa vitendo Laparoscopia.