Thursday, June 12, 2014

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AKIZINDUA TAMASHA LA VITABU VYA WATOTO MKOA WA DAR ES SALAAM



MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AKIZINDUA TAMASHA LA VITABU VYA WATOTO MKOA WA DAR ES SALAAM
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amesimama na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Katibu Tawala Ndugu Theresia Mbando (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (wa nne) nje ya jengo la Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanafunzi wa shule za msingi za Dar es Salaam wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa huo tarehe 12.6.2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam wakiwa wamebeba mabango yenye picha na ujumbe mbalimbali wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar zilizofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia mchezo wa sarakasi iliyokuwa ikichezwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ndugu Raymond Mushi (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya E & D, Ndugu Demere Kitunga (kushoto) wakati wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya sherehe za uzinduzi wa tamasha la vitabu vya watoto mkoani Dar tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiagana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Theresia Mbando mara baada ya kuzindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa terehe 12.6.2014.
Baadhi ya watoto walioshiriki uzinduzi wa tamasha la vitabu mkoani Dar es Salaam wakiwa wanasoma baadhi ya vitabu na majarida ya watoto wakati wa sherehe hizo kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha moja ya kijarida cha hadithi kwa ajili ya watoto alichokichagua kwa ajili ya kuwasomea hadithi watoto wakati akizindua rasmi Tamasha la vitabu vya watoto kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa hapa Dar Es Salaam tarehe 12.6.2014.
Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam, Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wakati wa uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Makumbusho terehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi mtoto Edda Kasika kutoka Shule ya Msingi Maktaba tuzo kwa kushika nafasi ya pili katika uandishi wa insha katika Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa tamasha la vitabu kwa watoto tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi washindi wa insha na mchapishaji wa vitabu bora vya watoto na wageni waalikwa mara baada ya kuzindua rasmi tamasha la vitabu vya watoto wa shule tarehe 12.6.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia maonyesho ya vitabu, vijarida na kazi mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa na wanafunzi wa shule za msingi mkoani Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la vitabu vya watoto tarehe 12.7.2014.