Saturday, June 14, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 14.06.2014.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 14.06.2014.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA TOFAUTI.

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDGAR PATRICK (24) MKAZI WA MAPOROMOKO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KILO 12 AMBAYO ALIIFICHA KATIKA NDOO YA PLASTIC.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 13:36 MCHANA KATIKA MTAA WA MAPOROMOKO, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

MSAKO WA PILI:

MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JACKSON EMANUEL (22) MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA NOTI BANDIA 17 ZA TSHS 10,000/= SAWA NA TSHS 170,000/= NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 60,000/=.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MAGEGE-ILEMI, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DW 5621984 – NOTI 17 NA NOTI 12 ZA TSHS 5,000/= ZIKIWA NA NAMBA BB 119382.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA ZAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI MATAPELI HASA KATIKA MAENEO YA BIASHARA PIA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA.

Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.