Saturday, June 14, 2014

Chuo cha Bahari-DMI cha saini makubaliano ya mafunzo ya ubaharia na UNRA(U)


Chuo cha Bahari-DMI cha saini makubaliano ya mafunzo ya ubaharia na UNRA(U)
Chuo cha Bahari (DMI) kimetia saini makubaliano ya mafunzo ya ubaharia na Mamlaka ya Barabara ya nchini Uganda (Uganda National Road Authority) Makubaliano hayo yalitiwa saini alhamisi 12.06.2014 jijini Kampala katika ofisi za UNRA zilizopo Lourdel rd plot 5 Nakasero.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari,Ing. Yassin M. Songoro , Mkuu wa Idara ya fedha,Bw. Mussa Kondo na Mkuu wa kozi fupi,Bw. Hilal Salum waliiwakilisha DMI na kwa upande wa UNRA Mkurugenzi Mtendaji,Bw. Ssebbugga Kimeze,Ing. Helbert Mutyaba waliwakilisha.

DMI ni chuo pekee cha Ubaharia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati kimepata fursa hiyo baada ya kushinda tenda iliyotangazwa na UNRA kupitia kitengo cha manunuzi (procurement),pia dmi imepewa fursa ya kufungua kituo cha mafunzo ya ubaharia Uganda ili kusaidia kutoa mafunzo hayo.

ombi hilo limeletwa hasa baada ya Uganda kuanza utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi.