Friday, June 13, 2014

SUMATRA MBEYA YABATILISHA MGOMO WA WAMILIKI WA DALADALA.


SUMATRA MBEYA YABATILISHA MGOMO WA WAMILIKI WA DALADALA.

 

Mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra) mkoani mbeya imelaani mgomo wa wamiliki wa mabasi madogo ya abiria maarufu kwa jina la daladala ambayo yanafanya safari zake kati ya stendi kuu na uyole jijini mbeya kwa madai kuwa mgomo huo  ni batiri huku ikiwaagiza wale ambao hawajarejesha magari yao barabarani kuanza kutoa huduma ya usafiri mara moja kabla mamlaka hiyo haijachukua hatua ya kufuta leseni zao.
Meneja wa sumatra mkoani mbeya ndiye ambaye ametoa tamko hilo ambapo amesema kuwa madai ya madereva wa mabasi hayo kuwa njia mpya ambazo zimeanzishwa na sumatra ni ndefu hayana msingi wowote kwa vile umbali uliopo haujazidi kiwango cha nauli kinachotozwa kisheria huku akiwataka madereva kurejesha huduma zao mara moja kabla hatua ya kufuta leseni zao hazijachukuliwa.

Katika hatua nyingine, Chacha amewaonya madereva na makondakta wenye nia ovu ya kuzuia wenzao wenye nia njema ya kutoa huduma, kuwa waache tabia hiyo kwa kuwa wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Kaimu mkurugenzi wa jiji la mbeya, Dk. Samwel Razaro amesema kuwa mgomo wa madereva wa mabasi hayo imeleta athari kubwa kwa wakazi wa jiji la mbeya na halmashauri, kutokana na mapato ya jiji kushindwa kukusanya mapato. 

Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala wa jia kuu ya uyole, sande mwakyusa, amesema kuwa baada ya kusikiliza uamuzi wa serikali anapeleka ujumbe huo kwa madereva wenzake ili waamue hatua zaidi za kuchukua.