Friday, June 13, 2014

NI SIMBA AU KONDOO? CAMEROON YAANZA VIBAYA KOMBE LA DUNIA, YACHAPWA 1-0 NA MEXICO

NI SIMBA AU KONDOO? CAMEROON YAANZA VIBAYA KOMBE LA DUNIA, YACHAPWA 1-0 NA MEXICO
NI SIMBA AU KONDOO? CAMEROON YAANZA VIBAYA KOMBE LA            DUNIA, YACHAPWA 1-0 NA MEXICO

WAWAKILISHI wa bara la Afrika kwenye michuano ya Kombe la Dunia, Cameroon wameanza vibaya kampeni zao baada ya kufungwa 1-0 na Mexico.

Cameroon walicheza soka bovu katika kipindi cha kwanza na kuonyesha wazi kuwa wanastahili kipigo.

Hata waliporejea kipindi cha pili, hawakuwa na jipya huku Mexico wakiendelea kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa. Kwa kifupi Cameroon wanajiita Simba wasiofugika, waligeuzwa kondoo na Mexico na pengine ni bahati kwao kufungwa bao 1 tu.

Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto'o hakuwa na madhara yoyote kwa Mexico.

Bao pekee la Mexico lilifungwa na Oribe Peralta katika dakika ya 61.