Tuesday, June 10, 2014

NHC yasaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya



NHC yasaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya
Shirika la Nyumba NHC leo limesaini mkataba na Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya ya Ujeni wa Nyumba 5,000 za garama nafuu.Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo mchana katika Hoteli ya New Dodoma mjini Dodoma na kuhudhuriwa na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Asiye na Wizara Maalum.

 Mhe.Prof Marck Mwandosya,Waziri, ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe MasharikiMawaziri mwingine aliyehudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Uchukuzi Mhe.Harrison Mwakyembe na kushuhudiwa na Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Mhe.Aggrey Mwanri.
Pichani wanaosaini kuanzia kulia ni kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi,Bw.Meckson Mwakipunga (Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya na Bw. Said Mderu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC,Bwa.Felix Maagi akibadilishana Mkataba na Mwekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga baada ya kutiliana saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela Bw.Meckson Mwakipunga akielezea kuhusu Mradi mzima, baada ya kutiliana saini Ujenzi wa nyumba 5,000 katika Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Asiye na Wizara Maalum. Mhe.Prof Marck Mwandosya. Waziri ambaye Wilaya hiyo Mpya iko katika Jimbo lake la Rungwe Mashariki akitoa shukurani baada ya mkataba Ujeni wa Nyumba 5,000 za garama nafuu kusainia.
Baadhi ya Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya wakifuatilia utiaji saini wa Mkataba wa Ujeni wa Nyumba 5,000 za garama nafuu katika Halmashauri ya Wilaya Mpya ya Busokela iliyopo Mkoani Mbeya.Picha na Deusdedit Moshi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati