KWELI Manchester United iliingia          mkenge kwa David Moyes baada ya kila kitu alichokifanya klabu          hapo kugeuka kuwa majanga.
        Baada ya kocha huyo kuisababisha          hasara kubwa ya kupoteza mamilioni ya pesa kutokana na kushindwa          kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya miamba hiyo ya Old Trafford          itapata hasara kubwa kwa kiungo wao Marouane Fellaini, ambaye          alisajiliwa na kocha huyo.
        Kocha Mkuu mpya wa kikosi hicho,          Louis van Gaal amesema haoni kama kiungo huyo anaweza kupata          nafasi kwenye timu hiyo msimu ujao na kwamba yupo sokoni kwa          pauni 15 milioni kitu ambacho kitaifanya Man United kuingia          hasara ya pauni 12.5 milioni.
        Fellaini alinunuliwa na Moyes          mwaka jana kwa ada ya pauni 27.5 milioni, lakini kwa msimu mzima          aliocheza kwenye kikosi hicho cha Man United hakufunga bao hata          moja kitendo kinachomfanya kocha mpya, Van Gaal afichue bayana          kwamba atakapoingia Old Trafford basi hamtaki mchezaji huyo.
        Kiungo huyo Mbelgiji kwa sasa          yupo kwenye fainali za Kombe la Dunia na kikosi cha Ubelgiji          nchini Brazil na kitu kipekee kitakachomfanya aendelee kubaki          Old Trafford msimu ujao kama atafanya kweli kwenye fainali hizo.
        Hata hivyo, licha ya Man United          kukubali kumuuza kwa hasara, hakuna klabu yoyote iliyojitokeza          kutaka kumsajili kiungo huyo kitendo kijachothibitisha kwamba          mzigo huo bado unaikabili timu hiyo.
        
 
