Mke wa Rais na Mwenyekiti wa                Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete                akisalimiana na Rais wa Shirika la International Health                Partiners (IHP)-JEMA Tanzania, Mama Mary Ellen Kitundu                mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Zinga huko                Bagamoyo, mkoani Pwani. Mama Salma alikwenda kijijini hapo                kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la hospitali ya watoto                inayojengwa na Shirika la IHP-JEMA Tanzania tarehe                10.6.2014. Katikati ni Mkurugenzi wa Mradi huo Dkt. Jesse                Kitundu.
                Mke wa Rais Mama Salma Kikwete                akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed                Kipozi wakitembelea eneo linalojengwa hospitali ya watoto                itakayo kuwa na uwezo wa vitanda 500 katika kijiji cha                Zinga huko Bagamoyo tarehe 10.6.2014.
                Mke wa Rais Mama Salma Kikwete                akizungumza na wageni waalikwa na wananchi wa Kijiji cha                Zinga wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la                hospitali ya watotot itakayokuwa na uwezo wa vitanda 500                tarehe 10.6.2014.
                        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete                akifungua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa jiwe la                msingi la ujenzi wa hospitali ya watoto katika Kijiji cha                Zinga huko wilayani Bagamoyo tarehe 10.6.2014. Kushoto kwa                Mama Salma ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed                Kipozi.
                        Mke wa Rais Mama Salma Kikwete                akipanda mti kwenye eneo linalojengwa hospitali ya watoto                katika kijiji cha Zinga wilayanI Bagamoyo mara baada ya                kuweka jiwe la msingi tarehe10.6.2014.
                Mke wa Rais Mama Salma Kikwete                akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali,                shirika la IHP-JEMA Tanzania na viongozi wa Kijiji cha                Zinga mara baada ya sherehe ya kuweka jiwe la msingi la                ujenzi wa hospitali ya watoto kijijini hapo tarehe                10.6.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.
         
