Friday, June 13, 2014

Mchemsho mwingine wa refa washuhudiwa wakati Mexico ikiibanjua Cameroon bao 1-0 leo



mchemsho mwingine wa refa washuhudiwa wakati Mexico ikiibanjua Cameroon bao 1-0 leo
Mshambuliaji Oribe Peralta wa Mexico amehakikisha kwamba haki inatendeka katika michezo ya awali ya Kombe la dunia alipoiwezesha nchi yake kuifunga Cameroon bao 1-0 jioni huu mjini Natal wakati michuaono hiyo ikiwa katika hatihati ya kashfa ingine ya uamuzi mbovu. 
Endapo kama Mexico wasingeshinda ni hakika Refa huyo kutoka Colombia Wilmar Roldan angekuwa katika wakati mgumu baada ya kukataa magoli mawili ya wazi ya timu hiyo kwa madai kuwa ni ya kuotea baada ya mchezaji wa zamani wa Tottenham Giovani dos Santos kutingisha nyavu za Cameroon mara mbili katika kipimdi cha kwanza. 
Ndio kusema refa huyo na FIFA walipata ahueni ya aina yake baada ya Mexico iliyotaewala mchezo ilipozawadiwa goli safi la siku, baada ya kipa wa Cameroon kupangua mkwaju wa Dos Santos na kumwekea Peralta aliyetumbukiza ngoma kimiani 
 Matokeo hayo yanaifanya Mexico kuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele pamoja na Brazil katjka kundi lao la A . Wababe hawa wawili (Mexico na Brazil) wanakutana siku ya Jumanne katika mji wa Fortaleza.
Kocha wa Mexico  Miguel Herrera akimpa maneno yake Refa kutoka Colombia Wilmar Roldan wakati wa mapumziko kwa kuwabania mabao mawili kipindi cha kwanza

Oribe Peralta akimchenga Samuel E'too kuifungia Mexico bao katika dakika ya  61 ya mchezo



Oribe Peralta akishangilia bao la Mexico dhidi ya Cameroon