Tuesday, May 27, 2014

SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAARIFA YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE


SOMA TAARIFA KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:TAARIFA YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
 
UTANGULIZI
Mnamo tarehe 27 Januari 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya dengue katika Kliniki ya 'International School of Tanganyika' iliyopo Manispaa ya Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam. Taarifa hiyo ya awali ilionyesha kuwepo kwa jumla ya wagonjwa 6 katika kituo hicho bila vifo.

Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na
ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013,  wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
  1. UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes. Dalili za ugonjwa huu ni homa ya ghafla,mwili kuchoka,  kuumwa na viungo, kuvimba tezi na kupatwa na harara. Uwepo wa homa, kuumwa kichwa  maumivu ya viungo na uchovu ndio dalili kuu  za ugonjwa huu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati  siku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukiwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine  dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria. Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;
    

    

    

Aina ya pili na ya tatu ni aina zenye dalili mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa na hatimaye kusababisha kifo. Kwa Tanzania, hadi sasa ni aina ya kwanza ya Homa ya Dengue imeripotiwa.

Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu  baada ya kuumwa na mbu aina ya "Aedes". Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.

Ugonjwa huu hauenezwi moja kwa moja kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bali kwa kupitia  mbu aliyeambukizwa na virusi vya homa ya dengue anapomuuma binadamu. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna tiba maalum ya kutibu virusi vya denge wala chanjo  bali mgonjwa anatibiwa kutokana na  dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue:

 
 
 
*Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
 
* Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
* Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo yaharuhusu maji kutuma
 
* Funika mashimo ya maji taka  kwa mfuniko imara
*Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama

o   Kujikinga na kuumwa na mbu
*  Tumia dawa za kufukuza mbu "mosquito repellants"
* Vaa nguo ndefu
*  Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (hasa kwa wale wanalala majira ya mchana)
* Weka wavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi

2. HALI HALISI YA SASA YA UGONJWA NCHINI

11.1  Idadi ya Wagonjwa:
Kuanzia tarehe 27 Januari hadi tarehe 6 April 2014, jumla ya wagonjwa 399 (Kinondoni – 322, Ilala – 61 na Temeke – 16) wamethibitishwa  kuwa na ugonjwa homa ya dengue.  kati yao, wagonjwa wawili (2) wamepoteza maisha;

(i)  Mwanamke, umri miaka 22, aliyefariki katika Hospitali ya Mwananyamala tarehe 14.3.2014.

(ii) Mwanamke, umri miaka 37, muuguzi, aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Temeke ambaye alifia hospitali ya MNH

11.2  Maeneo yaliyoathirika

Ugonjwa huu umeripotiwa katika kila eneo la Dar es salaam lakini Kata zilizoathirika zaidi kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi ni kama zifuatatazo;

KATA
IDADI
Msasani
93
Masaki
68
Magomeni
54
Kinondoni A/B/Manyanya
29
Mikocheni
21
Buguruni
20
Tandale
15
Sinza/Kijitonyama
13

11.3  Dalili za kuu zilizojitokeza
Wagonjwa wote 399 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa walikuwa na  na homa kali..  Aidha 82% ya wagonjwa walionyesha pia dalli ya kuumwa kichwa. Dalili nyingine ni zilizojitokeza ni pamoja na kutapika, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo,  na kuumwa tumbo.

11.4  Jinsia na Umri
Kati ya Wagonjwa 376, 214 (54%) walikuwa wanaume na 185(46%) walikuwa ni wanawake. Idadi kubwa ya wagonjwa waliothibitika kuwa na ugonjwa huu wako katika Umri zaidi ya miaka 16 yaani  asilimia 92. Aidha watoto chini ya umri wa miaka 5 walikuwa ni asilimia 2 tu.

 
Mlipuko huu wa tatu wa dengue hapa nchini ulianza tarehe 2 Januari 2014. Ongezeko kubwa la wagonjwa limejitokeza katika mwezi wa tatu (3) mwishoni na kushika kasi mwezi wa Aprili, 2014 ambapo wagonjwa wengi wameongezeka.

Jedwali No 1: Mwenendo wa Ugonjwa wa Dengue kuanzia utokee,2  Januari 2014- 6 May 2014 (N=399)
  1. HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA
 
*WAUJ imetoa  tamko la Serikali kwa wananchi kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari
 
 tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014.  Aidha, uelimishaji kwa wananchi 
 
unaendelea kupitia Radio, TV na magazeti. Aidha matumizi ya Vipaza sauti katika 
 
ngazi za chini utaanza na kusimamiwa na Halmashauri za Wilaya mkoani Dar es 
 
salaam.  

*Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga 
 
Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia
 
 inajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), 
 
"Ukweli Kuhusu Ugonjwa"(Fact sheet)  na mwongozo wa uchukuaji wa sampuli 
 
na matibabu. 
 

* Kuendelea kutoa elimu kwa Watumishi wa afya madaktari pamoja na 
 
wanaofanya maabara kuhusu namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha 
 
watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke 
 
wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado yanaendelea  kutolewa kupitia 
 
mikutano ya kila asubuhi ya kiltaaluma (Clinical meetings). Halmashauri 
 
zinaendelea pia kuyatoa mafunzo haya katika ngazi za chini.
 
 
 

*Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.



  Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika 
 
Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na 
 
Temeke Hospitali), aidha, Kituo cha ' International School of Tanganyika – IST' 
 kilichopo Manispaa ya Kinondoni pia kinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu 
pamoja na Kituo cha Hospital ya Muhimbili.
 
*Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya 
Taifa (NHLQATC) ambapo mpaka sasa kumethibitishwa kuwepo kwa aina 2 za 
virusi hivi yaani DENV2 na DENV3. Vile vile Wizara imepeleka kiasi kidogocha 
 
vipimo vya awali yaani "Dengue Rapid Test Kits" kwa baadhi ya vituo vya Dar 
 
es salaam kuimarisha utambuzi na vituo hivo ni pamoja na Muhimbili, Amana 
 
hospital, Mwananyamala hospitali, Temeke Hospital, na IST kliniki.
 
 
*Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa 
 
 
(saveilensi) ya IDSR . Aidha,  Wizara imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu 
 
wa mikoa na wilaya kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa 
 
za kila wiki (Infectious disease week ending).


*Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani 
 
kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri 
 
anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi 
 
wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
 
 
Kudhibiti mbu kwa kupulizia dawa ( Fogging) katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam. Aidha mpango wa WAUJ ni kufikia maeneo mengi zaidi pamoja na kufanya kuweka dawa ya kuua viliwi luwi (Larviciding)" kwa viluwiluwi.


*Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama 
 
mwongozo wa Kimataifa uvyaoelekeza.

* Kupitia Timu ya Taifa ya Maafa, Wizara imeandaa  mpango kazi na mkakati 
 
wa muda mfupi wa namna ambavyo ugonjwa huu utadhibitiwa ukishirikisha 
 
wadau mbalimbali. Kimabatanisho namba 1 kinafafanua kazi zilizoaninishwa.
 

3.2 Hatua za muda mrefu
*  WAUJ imeandaa Mpango Mkakati (2014 – 2018) wa kukabiliana na magonjwa ya 'Viral Haemerrhagic Fevers' ikihusisha na ugonjwa wa homa ya dengue.*  Halmashauri za mkoa kutengeneza "strategic plan" ya kwao kwa kuangalia "prototype plan" ya WAUJ

  1. Changamoto
 

 

 

 

 

Kiambatanisho namba 1,
MAAZIMIO YA KIKAO CHA TIMU YA TAIFA YA MAAFA KUHUSUIANA NA DENGUE FEVER

TAREHE 7.5.2014
Kazi
Shughuli
Mhusika
Muda wa Utekelezaji
Uratibu wa shughuli za Dengue Kitaifa
Kuwasilisha mpango kazi ulioandaliwa kwa ngazi za juu ili pia uweze kuwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu
WAUJ: Epidemiolojia
Mara moja
Uratibu wa shughuli za Dengue mkoani Dar es salaam
Kuandaa mpango mkakati wa namna ya kukabiliana na Dengue kwa kutumia prototype plan ya mpango mkakati wa Kitaifa
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Tarehe 12.5.2014
Udhibiti wa Mbu na viluwiluwi
Kuua mazalio ya mbu yaani viluwili (Larvidicing) kwa kutumia bio-larvicide –ambao iko kwa kiasi iliyokuwa inatumika katika mradi wa Bio larvicide kati ya Cuba na WAUJ kupitia NMCP. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Kuendelea na kufanya fogging (kuua mbu wapevu) wenye tayari vimelea kutumia viautilifu vya  kuua mbu katika maeneo yaliyotoka idadi ya wagonjwa wengi. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za mitaa na CORPS
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja (Angalizo: utategemea pia hali ya hewa na mvua)

: Maafisa Afya wote wa Halmashauri  watahusika katika kusimamia na kuhamasisha usafi wa mazingira kwa kutumia sheria ndogo ndogo ilizojiwekea ikiwemo na kutoa faini
WAUJ: Kitengo cha Usafi wa Mazingira
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja

Maafisa Afya  ikiwemo wa kata wataelemisha  wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa kwa  vipaza sauti, uongozi wa mitaa, kugawa vielemishi. Na vilevile kuendelea kutumia vyombo vya habari na TV
WAUJ: Kitengo cha Usafi cha mazingira na Elimu ya Afya
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke

Elimu kwa watumishi wa Afya
Kutoa elimu kupitia clinical meetings katika hospitali zote za wilaya na pia kupitia APHTA
WAUJ: Epidemiolojia
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha utambuzi wa ugonjwa
WAUJ kuwasiliana na MSD kuhusu upatikanaji wa "Dengue Rapid Kits" ili Halmashauri ziweze kufuata utaratibu wa manunuzi
Halmashauri na pia MNH kupanga katika mipango yao fedha za kununua kits hizi
Kwa kipindi hiki ambapo "kits" zinaonekana kupungua katika maeneo tajwa yaani MNH, na Hospital za Wilaya mkoani Dar es salaam, NHLQATC itatumika kupima vipimo hivi ili kuwepo na mwenendelezo wa "Sentinel Surveillance"
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Halmashauri 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa
Kutengeneza protocol ya Surveillance pamoja na alogarithm ya matibabu
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
10.5.2014

Kuweka "messages" katika Point of Entry
WAUJ: Kitengo cha Afya ya Mazingira
Mara moja
Ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa huu
WAUJ kuandika barua kwa RAS Dar es saalam kuanisha maeneo ya utekelezaji ambao yako chini ya mamlaka yake
WAUJ kuandika barua ya kuomba  zaidi msaada wa "Dengue Rapid Kits" WHO, CDC na USAID
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
WAUJ: Epidemiolojia na Diagnostic
Mara moja

UNICEF kusaidia na IEC materials yaani Posters na leaflets ambazo tayari zimeshatengenezwa
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
Mara moja maana tayari kuna mawasiliano

WHO kusaidia katika uelimishaji kwa kupitia kifungu cha fedha za "World Health Day" iliyolenga masuala ya "vector"
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya Afya kwa Umma
Utekelezaji unategemea barua kuandikwa kutoka WAUJ kwenda WHO

Imeandaliwa na:
Kitengo cha Epidemiolojia na Ufuatiliaji wa Magonjwa
May, 2014