Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Mhe. Nguyen Phuong Nga mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mhe. Nguyen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Mhe. Dkt. Maalim na Mhe. Nguyen wakizungumza huku Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vo Thanh Nam (kushoto), Bw. Nathaniel Kaaya (kulia), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia na Bw.Emmanuel Ruangisa, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo.