Friday, October 19, 2012

Taswira Rasmi Jinsi Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania Walivyotinga Mitaani Leo Jijini Dar es Salaam Kutuliza Fujo na Maadamano Leo


  Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. 
 Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikuu
   Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza
 Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo

 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo


  Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki
   Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo
   Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo
   Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo
  Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.Picha zote na Happiness Mnale