Friday, October 19, 2012

WANANCHI WATEKETEAZA MATREKTA KATIKA SHAMBA LINALOMILIKIWA NA KANISA LA EFATHA HUKO SUMBAWANGA



Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao
walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba
hilo.

Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara liyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani. (Picha na Joshua Mwakabungu-Sumbawanga)