PRETORIA, Afrika Kusini
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameingia kwenye kashfa ya ufujaji wa fedha za Serikali yake kutokana na kutarajia kufanya ukarabati wa jumba lake la kifahari kwa gharama ya dola milioni 25 sawa na zaidi ya Bilioni 3 za Kitanzania.
Taarifa za nchini humo zinaeleza kuwa, ukarabati huo wa jumba lake gharama zake zote zinatarajiwa kulipwa na serikali.
Kufuatia hatua hiyo, uchunguzi umeanza kuhusu ukarabati huo ambao ni nyumba yake binafsi Rais Jacob Zuma.
Tangazo limetolewa na ofisi ya Mhifadhi wa Masilahi ya Wananchi, baada ya magazeti kutuhumu kwamba ukarabati unaopangwa kufanywa kwenye nyumba ya Rais Zuma utaogharimu dola milioni 25, karibu wote unatarajiwa kulipwa na serikali.
Msemaji alieleza kuwa kamati ya uchunguzi imewasiliana na ofisi ya rais kuhusu ujenzi huo kwenye nyumba ya Rais Zuma ilioko Nkandla katika jimbo la KwaZulu-Natal.
Hata hivyo Serikali yake imetetea uamuzi huo na kueleza kwamba ujenzi huo unafuata kanuni rasmi.Source:BBC Swahilli