Monday, October 01, 2012

PICHA ZA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA CCM MANISPAA YA SINGIDA ULIOFANYIKA KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA VETA.




 Mgombea nafasi ya NEC manispaa ya Singida Hussein Mazala akielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mahali uchaguzi mkuu wa CCM manispaa ya Singida unaofanyka leo ili kuomba kura.

Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa CCM manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami,akitoa maelekezo ya zoezi la uchaguzi huo uliofanyika kwenye kumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
 
Mgombea nafasi ya NEC manispaa ya Singida, Hussein Mazala (kushoto) akipeana mkono na mpinzani wake Diya Kiya.

Mgombea  nafasi ya NEC manispaa ya Singida Hussein Mazala,akijinadi mbele ya wajumbe wa mkutano huo (hawapo kwenye picha).
Mbunge wa jimbo la Singida mjini na MNEC mkoa wa Singida,Mohammed Gullam Dewji,akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi CCM manispaa ya Singida uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone (wa pili kulia) akifuatilia zoezi la mkutano mkuu wa uchaguzi wa CCM manispaa ya Singida,uliofanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA.
Mwenyekiti CCM mkoa wa Singida anayemaliza muda wake Joramu Allute (wa kwanza kulia) akifuatilia kwa makini zoezi la uchaguzi mkuu wa manispaa ya Singida.Wa kwanza  kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na anayefuatia ni mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji.
Mgombea nafasi ya NEC (CCM) manispaa ya Singida Hussein Mazala akitoka nje ya ukumbi wa mikutano mahali uchaguzi mkuu unaofanyika baada ya kumaliza kujinadi.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi katika jimbo la Singida mjini unaoendelea (sasa) kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.