Wednesday, October 17, 2012

hafla ya chakula cha jioni kwa wadau wa Kongamano la Kwanza la Afrika kuhusu Usimamizi wa Utalii Endelevu katika Hifadhi za Taifa yafana jijini arusha



Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiwakaribisha wageni mbali mbali katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Wizaza yake washiriki wa Kongamano la Kwanza la Afrika kuhusu Usimamizi wa Utalii Endelevu katika Hifadhi za Taifa iliyofanyika katika hoteli ya Kibo Palece,Jijini Arusha na kuwashirikisha wadau wa utalii pamoja na mawaziri kutoka nchi 13 Barani Afrika.
Baadhi ya Wageni walioshiriki wa Kongamano la Kwanza la Afrika kuhusu Usimamizi wa Utalii Endelevu katika Hifadhi za Taifa iliyofanyika katika hoteli ya Kibo Palece,Jijini Arusha,wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki (hayupo pichani).
Kikundi cha Ngoma za Asili cha Jijini Arusha kikitumbuiza katika hafla ya chakula cha usiku kilichoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii,Arusha.