Friday, October 05, 2012

BENKI YA DCB YATANUA WIGO WA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA NCHINI.



Mhe. Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akizungumza wakati wa Sherehe ya Miaka 10 ya Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam (DCB) ambapo amewafafanulia wananchi kuwa Benki hiyo iliweka na kutekeleza mikakati ya kukuza mitaji ili kuendesha shughuli za kibenki vizuri na kuongeza gawio kwa wanahisa wake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Wananchi wa Dar es Salaam BaloziPaul Rupia akitoa hotuba katika maadhimisho ya Sherehe ya Benki hiyo Kutimiza miaka 10 ambapo amesema baada ya kuongezeka kwa mtaji hadi kufikia shilingi bilioni 16, Benki hiyo imeona ni vizuri ikatanua zaidi wigo wa utoaji huduma kwa wateja wake na kukaribiana na ushindani katika tasnia ya benki.

Baadhi ya ya Wakurugenzi wa Bodi ya Benki ya Biashara DCB wakimsikiliza kwa makuni Balozi paul Rupia akitangaza kuwa Benki hiyo sasa aimeamua kubadili jina na hadhi yake kutoka ‘Benki ya Wananchi’ na kuwa Benki Kamili ya Biashara.