Moja kati ya sababu zilizopelekea kwa wananchi wa Jimbo la kisesa kumtunuku Rais Kikwete Hati ya Kasi ya Maendeleo ni kitendo cha kutimiza ahadi ya kulipatia jimbo hilo umeme, Uimarishwaji na uboreshwaji wa huduma za Elimu, Afya na Barabara pamoja na hivi karibuni Serikali kuahidi kutoa kiasi cha 6M/- kulipa fidia ya ng’ombe 22 wanaodaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa pori la akiba Maswa wilayani Meatu, mkoani Simiyu.
Inadaiwa ng,ombe hao walipigwa risasi na kuuawa Desemba 2009 baada ya kuingizwa kuchungia ndani ya hifadhi hiyo, kitendo ambacho ni kinyume na sheria zinazolinda hifadhi za wanyama pori.
|