Friday, September 21, 2012

MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA



  Wananchi wengi wa Mkoa wa Rukwa walihasika kuulaki Mwenge huo wa Uhuru kwani wengine walilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kupanda juu ya miti ili waweze kuuona Mwenge huo.
 Baadhi ya wananchi Mkoani Rukwa waking'ang'ania kushika mwenge wa uhuru kabla ya Mwenge huo kuondoka kuelekea kuanza mbio zake Mkoani Katavi hapo jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa ambapo Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.
 Mwenge wa Uhuru ukipewa heshma ya mwisho kwa stali ya mchakamchaka kabla ya kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kumaliza mbio zake mkoani humo jana, Wakijumuika kwenye gwaride hilo la utii kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddy Kimanta, Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Capt. Honest Mwanossa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Capt. Honest Erenest Mwanossa akiagana na viongozi wa Mkoa wa Rukwa mara baada ya kukamilisha jukumu zito la kukimbiza mwenge katika Wilaya tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Alieshikana nae mkono na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkasi wakiwa wamebeba bango lililokuwa na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru. Ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu kitaifa ni Mabadiliko ya Katiba Timiza Wajibu Toa Maoni yako na Mapambano dhidi ya Ukimwi na Dawa za kulevya.
Muongozaji wa Blog ya Rukwareview Mr. Temba (shoto) akishare Photo na Mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu Kajia Godfrey kutoka Shinyanga kabla ya kumaliza mbio hizo Mkoani Rukwa jana.Picha na Habari zimeletwa hapa na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa