Monday, September 17, 2012

UJERUMANI YAMPIGA MARUFUKU MCHUNGAJI TERRY JONES WA MAREKANI KUINGIA BERLIN.




Serikali ya Ujerumani imemkataza mchungaji Terry Jones (pichani) mwenye msimamo mkali wa kidini kutoka Marekani  kuingia mjini Berlin kufuatia maandamano katika nchi za kiislamu yaliyosababishwa na filamu inayoudhalilisha Uislamu.
Akizungumzia mipango ya kundi lenye msimamo mkali kumualika mchungaji huyo kutoka Florida kutembelea Ujerumani, Msemaji wa wizara hiyo amesema ziara ya Jones itakuwa kinyume na azma ya kudumisha amani ya umma.
Mchungaji  Jones aliyesababisha maandamano makubwa kwa mipango yake ya kuichoma Quran hadharani, amesema filamu hiyo haikulenga kuwatusi Waislamu.
Inaripotiwa kwamba kundi hilo dogo linalojiita “Pro Deutschland” linataka kuandaa maonyesho ya filamu hiyo mjini Berlin.