Monday, September 17, 2012

WIZI WA KAZI ZA WASANII WAMFIKISHA KIZIMBANI RAIA WA UFARANSA BAADA YA KU-’DOWNLOAD’ NYIMBO ZA RIHANNA.




Raia mmoja nchini Ufaransa Alain Prevost amekuwa mtu wa kwanza kupigwa faini na mahakama chini ya sheria mpya za nchi hiyo za kuzuia wizi wa kazi za wasanii.
Prevost amepigwa faini ya Euro 150 kwa kuiba nyimbo mbili za Rihanna kupitia mtandaoni ‘Download’ japokuwa mkewe amekiri kuwa yeye ndie aliye’download’ nyimbo hizo.
Hata hivyo faini hiyo imeelekezwa kwa Prevost mwenye umri wa miaka 40 kwa kuwa kumbukumbu zinaonyesha yeye ndiye aliyelipia bili ya mtandao uliotumika kuibia nyimbo hizo.
Wakala wa Serikali ya Ufaransa unaosimamia sera ya kuzuia wizi wa kazi za wasanii nchini hiyo tayari unaandaa kesi dhidi ya watu wengine 14 wanaotuhumiwa kuiba kinyemela miziki na filamu katika mitandao.