Tuesday, September 18, 2012

Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar yaitembelea Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania


 Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Baraza hilo Bw. Ally Abdallah Ally (wa pili kushoto) akioneshwa jinsi Makataba mtandao ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania inavyofanya kazi, wa pili kulia nyuma ni Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Beatrice Korosso.
 Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Profesa Ibrahim Juma akimkabidhi Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Ally Abdallah Ally baadhi ya Ripoti zilizofanyiwa kazi na Tume..
 Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Profesa Ibrahim Juma akiandika baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na wajumbe wa kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Baraza la wawakilishi.
Wajumbe wa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala wa Baraza la Wawkilishi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Profesa Ibrahim Juma, akifuatiwa na Naibu Spika wa Baraza la wawakilishi Mh. Ally Abdallah Ally na Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Beatrice Korosso